Kitaifa

Kado arejea nyumbani kumrithi Nduda

on

MLINDA mlango Shaban Kado amerejea nyumbani baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar akitokea Mwadui FC ya mkoani Shinyanga.

Kado ametokea Mtibwa ambapo baada ya kuonyesha ubora mkubwa katika misimu kadhaa iliyopita alijiunga na timu ya Yanga kabla ya kujiunga na Mwadui iliyokuwa chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ wakati huo.

Shaban Kado akisaini mkataba mbele ya Jamal Bayser

Kado anajiunga na Mtibwa kwa mkataba wa miaka miwili kuchukua mikoba iliyoachwa wazi na mlinda mlango Said Mohammed ‘Nduda’ ambaye jana alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba.

Nduda yupo kwenye kiwango bora kwa sasa kilichomfanya awemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambapo katika michuano ya COSAFA iliyofanyika nchini Afrika Kusini mapema mwezi huu.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *