Kitaifa

Kagere Noma, Aipeleka Gor Mahia Fainali SportPesa

on

MSHAMBULIAJI mkongwe Medie Kagere ameipeleka timu yake ya Gor Mahia fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Nakuru All Stars katika mchezo wa nusu fainali uliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.

Kagere alifunga bao hilo dakika ya 45 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na George Odhiambo upande wa kushoto huku mabeki wa Nakuru wakishindwa kuondoa hatari hiyo.

Kagere ndiye kinara wa ufungaji katika michuano hiyo baada ya kufikisha mabao matatu kufuati mawili aliyofunga dhidi ya Singida United katika ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa awali.

George Odhiambo akishangilia bao lake

Michuano hiyo iliyokuwa inashirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya na kushuhudiwa timu za AFC Leopards na Gor zote za Kenya zikitinga fainali itakayo fanyika siku ya Jumapili katika uwanja huo.

Odhiambo aliipatia Gor bao la pili dakika ya 81 baada ya kutokea piga ni kupige langoni mwa Nakuru kufuatia shambulizi lililoanzishwa na Oliver Maloba upande was kushoto.

Fainali ya michuano hiyo inazikutanisha timu zenye ushindani mkubwa nchini Kenya ‘Kenya Derby’ kitu ambacho kitaongeza hamasa ya mchezo huo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *