Kitaifa

Kama Mlidhani Utani, Habari Ndio Hii

on

SI tetesi tena ni rasmi! Emmanuel Okwi ataitumikia timu ya Simba katika michuano mbalimbali ya ndani na ile ya kimataifa kuanzia msimu ujao.

Okwi amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa kombe la FA mbele ya Makamu wa Rais wa klabu hiyo Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na mwanachama maarufu bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’ usiku huu.

Raia huyo wa Uganda aliwasili nchini jana usiku ambapo ilitarajiwa kusaini mkataba mchana wa leo lakini mazungumzo baina yake na viongozi yalikuwa hayajakamilika na hatimaye usiku huu akakamilisha dili hilo.

Okwi akiwa na Mohamed Dewji ‘Mo’

Okwi anaungana na nyota wengine kama John Bocco ‘Adebayor’, Shomari Kapombe, Ally Shomari, Jamal Mwambeleko, Yusuph Mlipili na Emmanuel Mseja kwa ajili ya kuwatumikia Wekundu hao msimu ujao.

Simba inaandaa kikosi imara kwakua mwakani itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *