Kitaifa

Kamati ya Utendaji TFF Kukutana Kuhusu Sintofahamu ya Uchaguzi

on

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF itakutana Julai 4 kwa ajili ya kujadili suala la Kamati ya Uchaguzi kusitisha mchakato wote wa Uchaguzi kutokana na mgawanyiko baina ya wajumbe.

Kaimu katibu mkuu wa (TFF), Salum Madadi alisema wamepokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho hilo Wakili Revocatus Kuuli kuhusu kusitisha mchakato huo kutokana na wajumbe kutofautiana ambapo mpaka sasa majina ya wagombea hayajapitishwa.

“Kamati ya Utendaji itakutana Julai 4 kujadili suala hilo. Kuna mgawanyiko umejitokeza miongoni kwa wajumbe hivyo ni rasmi mchakato wote wa Uchaguzi umesimamishwa,” alisema Madadi.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Wakili Revocatus Kuuli

Mapema Wakili Kuuli aliongea na Waandishi wa Habari kuhusu kusitisha mchakato huo ambapo alisema imetokana na mgawanyiko uliojitokeza baina ya wajumbe ambao wanaonyesha kupendelea baadhi ya wagombea.

“Mchakato wa Uchaguzi umesimamishwa mpaka Kamati ya Utendaji itakapokutana Jumanne ijayo,” alisema Kuuli.

Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika mkoani Dodoma Agosti 12 huku zoezi la usaili kwa wagombea likikamilika jana.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *