Kitaifa

Kamati ya Utendaji Yaitumbua Kamati ya Uchaguzi TFF

on

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imewaengua wajumbe wote wa Kamati ya Uchaguzi isipokuwa Mwenyekiti Revocatus Kuuli anayeendelea kubaki kwenye nafasi yake.

Julai 2 Kamati ya uchaguzi kupitia kwa Mwenyekiti wake Wakili Kuuli ilitangaza kusitisha mchakato wa uchaguzi kutokana na mgawanyiko uliojitokeza baina ya wajumbe kwa sababu ya kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwa kufikia muafaka kwenye zoezi la usaili.

Kaimu katibu wa TFF Salum Madadi amewaambia Waandishi wa Habari kuwa wamefanya mabadiliko katika kamati ya uchaguzi kwa kumbakiza Kuuli pekee na kuongeza wengine.

Salum Madadi, Kaimu katibu Mkuu TFF

Madadi amewataja wajumbe walioondolewa kuwa ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Domina Madeli, Juma Lalika, Jeremiah Wambura na Omari Hamimu huku walioongezwa wakiwa ni makamu mwenyekiti Mohammed Mchengela, Wakili Kiomon Kibamba, Malangwe Ally na Thadeus Karua.

“Kamati ya Utendaji imekutana na kufanya mabadiliko katika kamati zake mbalimbali kutokana na mapungufu yaliyojitokeza ikiwemo kamati ya uchaguzi.

“Kamati hiyo ya uchaguzi itakutana kesho kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali na kuendelea na mchakato wa uchaguzi,” alisema Madadi.

Uchaguzi wa TFF utafanyika katika tarehe ile ile iliyopangwa ya Agosti 12 mkoani Dodoma.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *