Kitaifa

Karia Awekewa Pingamizi Uchaguzi TFF

on

WAGOMBEA wawili akiwemo Makamu wa Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia wamewekewa pingamizi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mkoani Dodoma.

Karia ambaye anagombea nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo amewekewa pingamizi na John Kijumbe huku Mussa Sima anayewania ujumbe akiwekewa pingamizi na Hussein Mwamba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho hilo Wakili Revocatus Kuuli alisema katika wagombea wote waliojitokeza katika nafasi mbalimbali ni hao wawili ambao wamewekewa pingamizi huku zikishindwa kusikilizwa kutokana na wahusika kutokuwepo kwa muda uliopangwa.

“Wagombea wawili wamewekewa pingamizi ambao ni Karia (Urais) na Sima (Ujumbe) lakini bado pingamizi hizo hajizasikilizwa kutokana na wahusika kuchelewa,” alisema Kuuli.

Zoezi la usaili kwa wagombea limeanza saa sita mchana ambalo litachukua siku tatu.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *