Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Kauli ya Katwila Baada ya Kumaliza Mkataba Mtibwa

0 275

KOCHA wa Mtibwa Sugar Zubery Katwila amemaliza mkataba wa kuwanoa wakata miwa hao na sasa huko huru kujiunga na timu yoyote akisema anawapa nafasi ya kwanza waajiri wake hao lakini endapo itatokea ofa nzuri zaidi ataondoka kwenye timu hiyo.

Katwila ambaye ameipa Mtibwa ubingwa wa kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) pamoja na kumaliza katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa kujikusanyia pointi 41, amesema kwamba atakaa chini na viongozi wake ili waweze kukubaliana.

Related Posts
1 of 32

“Mkataba kweli umeisha ila nina imani nitakaa chini na viongozi wangu kwa ajili ya mkataba. Mpira ni kazi yangu siwezi kusema sitaondoka, hapa ni nyumbani nimekaa muda mrefu lakini naweza kwenda kutafuta maisha mengine ni jambo tu la kuelewana.”

Mtibwa imekabidhi kombe la ASFC kwa wadhamini wao SuperDoll katika ofisi zao zilizopo barabara ya Mwalimu Nyerere jijini Dar.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...