Kitaifa

Kauli ya Mkude Baada ya Kutoka Hospitali

on

Kiungo wa Simba, Jonas Mkude ameruhusiwa mchana wa leo na kupewa masharti ambayo yatamfanya asijiunge na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ inayojiandaa na mechi dhidi ya Lesotho ambayo ni ya kuwania kufuzu fainali za Afcon.

Mkude ambaye kwasasa yupo nyumbani kwake Kimara Suca alipata ajali ya gari jana akitokea Dodoma ambako timu yake ilikuwa inacheza mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC alilazwa katika hispitali yaTaifa ya Muhimbili.

Kiungo huyo alipata ajali katika eneo la Dumila mjini Morogoro akiwa na gari aina ya Toyota Landcruser ambalo aliomba lifti kuwahi kambi ya Stars.

Mkude ameiambia BOIPLUS MEDIA kuwa hali yake haikuwa nzuri baada ya ajali hiyo ingawa kwasasa anaendelea vizuri lakini ameshauriwa kupata muda mrefu wa kulala ili kuepusha madhara ya kupooza mikono na miguu hapo baadaye akikiuka masharti hayo.

“Baada ya ajali kutokea nilijuwa kama sijaumia sana lakini muda ulivyokuwa unaenda maumivu yalizidi na kupoteza fahamu, sikutibiwa hospitali yoyote Morogoro bali likimbizwa moja kwa moja Muhimbili kwani kichwa kilianza kuvimba.

“Baada ya wiki mbili nitarudi hospitali na sasa siwezi kujiunga na Stars hadi hapo baadaye watakaporejea, nasikia maumivu ya mwili na siwezi kugeuka vizuri maana shingo linauma, nahitaji kupumzika kidogo ingawa hata ndani ya siku nne hii hali itakuwa imemalizika,” alisema Mkude.

Mkude alisema kuwa ajali hiyo ilitokana na kupasuka kwa taili la nyuma na gari ikiwa kwenye mwendo hivyo dereva kushindwa kufunga breki kwa haraka.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *