The sports Hub

Kauli ya Ulimwengu Baada ya Kutajwa Kutua Msimbazi

0 1,821

STRAIKA wa zamani wa TP Mazembe ya DR Congo aliyevunja mkatabana Al Hilal ya Sudan, Thomas Ulimwengu amevunja ukimya kwa kueleza msimamo wake baada ya habari kueneakuwa klabu ya Simba imeanza mchakato wa kuwania saini yake.

Akizungumza na BOIPLUS kwa njia ya simu akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ nchini Afrika Kusini, Ulimwengu alisema hakuna chochote kilichofikia hatua ya kukitolea maelezo na kwamba ataliweka wazi mara mambo yatakapokuwa tayari.

“Hakuna ninachoweza kusema kuhusu usajili wangu, akili yangu ipo timu ya taifa tu wakati huo hayo mengine yakiendelea huko. Kama kutakuwa na lolote nitaliweka wazi¬† ila kwasasa naomba mniache kwanza,’ alisema Ulimwengu.

Simba wapo katika mchakato wa kukiimarisha zaidi kikosi chao kwa lengo la kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa hivyo taarifa za kumhitaji Ulimwengu aliyewahi kutwaa ubingwa wa Afrika zimeonekana kubeba uzito.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.