Kitaifa

Kenny Ally Azitosa Yanga, Azam na Kutua Singida United

on

KIUNGO wa Mbeya City, Kenny Ally kesho anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili na Singida United jijini Dar es Salaam baada ya kuachana na ofa za Yanga na Azam FC waliokuwa wakimwania kwa nguvu.

Habari kutoka vyanzo vyetu ndani ya klabu za Singida na Mbeya City zinasema kiungo huyo ambaye tayari ameingia jijini jioni ya leo aliamua kuachana na Wagonga Nyundo hao baada ya kumaliza mkataba wake ingawa walikuwa tayari kumwongeza mkataba mpya.

Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kuwania saini ya kiungo huyo ‘Fundi’ lakini walishindwa kumalizana nae baada ya mabingwa hao kushindwa kukubaliana l na dau alilowatajia la sh 40 milioni.

Kiungo huyo aliingia kwenye orodha ya usajili wa Azam ambao jana walifanya mazungumzo lakini walishindwa kufikia makubaliano katika pesa ya usajili ambayo imedaiwa kuwa ni ndogo kuliko waliyotoa Singida United.

 

Usajili mkubwa unaofanywa na Singida unazidi kuvitia tumbo joto vigogo vya ligi kuu ya Vodacom huku kitendo cha kuingia mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa hapo jana kikiwa ni chachu kwa timu hiyo kufanya vema katika ligi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *