The sports Hub

Kessy Akamata Medali Yake ya Kwanza Zambia Nkana Ikitwaa Ubingwa

0 333

BEKI wa Nkana Red Devils ya Zambia, mtanzania Hassan Kessy leo amefanikiwa kutwaa taji lake la kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo miezi minne iliyopita.

Nkana wametwaa kombe la Barclays baada ya kuisambaratisha timu ya daraja la kwanza ya Young Buffaloes mabao 3-0 katika fainali iliyopigwa kwenye dimba la Mashujaa wa Taifa jijini Lusaka jioni ya leo.

Straika Ronald Kampamba aliifungia Nkana mabao mawili kipindi cha kwanza mbele ya Rais wa Zambia Edgar Lungu huku Walter Bwalya aliyeibuka mchezaji bora wa mechi hiyo akitupia la tatu mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Hassan Kessy

Nkana walionyesha nia ya kutwaa ubingwa huo kwa kuwachezesha nyota wao wote akiwemo Kessy na wengine kama Musa Mohammed, Joseph Musonda, Jacob Ngulube, Harrison Chisala na Richard Ocran.

Kutokana na ubingwa huo, Nkana wamejinyakulia kitita cha Kwacha 400,000 (zaidi ya sh 77 milioni) huku Buffaloes wakiambulia Kwacha 180,000 (sh. 35 milioni)

Get real time updates directly on you device, subscribe now.