Kitaifa

Kifaru Awapa Neno Wapiga Kura Uchaguzi TFF

on

KUELEKEA katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) wadau mbalimbali wa soka nchini wamekuwa na maoni tofauti kuhusu viongozi gani wanapaswa kuchukua hatamu kwa miaka minne ijayo.

Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu lilifungwa rasmi Juni 20 ambapo watu 74 wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali ambapo katika nafasi ya Rais wamejitokeza 10.

Msemaji wa timu ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru (pichani juu) ameshauri wapiga kura kuhakikisha wanachagua viongozi wenye uwezo wa kuliongoza soka kwa kulitoa lilipo na kulipeleka mbele zaidi kisha kulifanya lifahamike kimataifa.

Kifaru alisema wanahitajika viongozi ambao wataweza kutatua changamoto kama ubovu wa viwanja, usimamizi mzuri wa ligi, upangaji wa ratiba pamoja na waamuzi vitu ambavyo vimekuwa vikitia doa soka la Tanzania.

“Tunahitaji viongozi ambao wataweza kutatua changamoto zinazokabili soka letu, wenye nia ya dhati ya kututoa hapa na kutupeleka mbele sio wenye dhamira tofauti,” alisema Kifaru.

Kifaru alishindwa kuzuia hisia zake na kusema kama angekuwa ni miongoni mwa wapiga kura katika uchaguzi huo angemchagua Fredrick Mwakalebela katika nafasi ya Urais kwakua ana vigezo vya kuliongoza Shirikisho hilo.

Uchaguzi huo utafanyika Agosti 12 mkoani Dodoma huku Rais Jamal Malinzi akichukua fomu kutetea nafasi yake.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About William Kange

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *