Kitaifa

Kifaru Ayahusisha Mafanikio ya Stars na Mtibwa Sugar

on

UONGOZI wa klabu ya Mtibwa Sugar umelimwagia sifa benchi la ufundi la timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ chini ya kocha Salum Mayanga kwa mafanikio waliyopata kwenye michuano ya COSAFA iliyofanyika nchini Afrika Kusini huku wakiyahusisha moja kwa moja na klabu yao.

Stars ambayo imetua nchini usiku wa kuamkia leo imemaliza nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo na kuwashangaza wengi ambao hawakutarajia kitu hicho kutokea.

Msemaji wa ‘Wakata miwa’ hao Thobias Kifaru ameiambia BOIPLUS kuwa kocha Mayanga amejitahidi kuita wachezaji wazuri wasio na majina makubwa ambao wameweza kuliwakilisha vema Taifa huku wakijivunia uwepo wa nyota wengi waliopitia klabuni kwao.

Said Mohammed ‘Nduda’

“Ukiacha Mayanga na kocha wa makipa Patrick Mwangata wapo wachezaji kama Salim Mbonde, Stamil Mbonde, Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya, Said Mohammed ‘Nduda’ na Ramadhan Kessi, hao wote wamepitia katika mikono salama ya timu ya Mtibwa Sugar.

“Kwahiyo kama uongozi tuna sababu ya kujivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya timu yetu ya taifa,” alisema Kifaru.

Kuhusu maandalizi ya msimu mpya wa ligi Kifaru alisema wiki ijayo ndiyo watajua kama wataweka kambi jijini Dar es Salaam kama ilivyo kawaida yao au la kwakuwa bado uongozi haujafanya maamuzi.

“Kuhusu kambi hadi wiki ijayo ndiyo tutajua kama tutaweka Dar es Salaam au kwingineko na usajili unaendelea vizuri ukikamilika tutawapa taarifa,” alisema Kifaru.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *