Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Kiganja awapa neno waogeleaji na viongozi wao

0 69

WAOGELEAJI saba wanatarajia kuondoka jioni ya leo kuelekea nchini Morocco kushiriki mashindano ya kuogelea yatakayoshirikisha waogeleaji vijana kutoka shule mbalimbali duniani.

Akiwakabidhi bendera washiriki hao asubuhi ya leo, katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja amewataka kuiwakilisha vema nchi pamoja na kupanua wigo kwa michezo mingine nchi itakapokua inashiriki.

Related Posts
1 of 949

Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza mashindano haya ya shule kimataifa.

Timu ya waogeleaji

Kiganja pia ametoa wito kwa viongozi wengine wa vyama vya michezo kujitambua, kufanya kazi kwa misingi ya utawala bora na uwazi lakini pia kushirikiana na serikali badala ya kuitupia lawama.

Kwa upande wake kocha atakayeambatana na timu hiyo, John Belela amesema amewaandaa vijana hao vizuri na anatumaini watafanya vizuri katika mashindano hayo ya ISF.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...