Kitaifa

KIMENYA: Walioitwa Stars Hawanizidi Uwezo, Labda Mashabiki

on

Salum Kimenya (kulia) akiwa na mwandishi wa Boiplus, Bakari Kagoma

BEKI wa kulia wa timu ya Prisons, Salum Kimenya amesema amewazidi uwezo mabeki wanaocheza nafasi hiyo walioitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ila kwakuwa hachezi kwenye timu kubwa ndiyo maana anakosa nafasi ya kuitumikia timu hiyo ya Taifa.

Kikosi cha Stars kwa sasa kipo nchini Misri kwa ajili ya kambi ya siku nane kujiwinda na mchezo wa kufuzu michuano ya Afrika (AFCON) mwaka 2019 dhidi ya Lesotho mchezo utakaofanyika jijini Dar es Salaam, Juni 10.

Kocha wa timu hiyo, Salum Mayanga aliwaita kikosini Shomari Kapombe wa Azam na Hassan Kessy wa Yanga kwenye kikosi chake lakini Kimenya alisema nyota hao hawajamzidi uwezo ila wanabebwa na ukubwa wa klabu zao.

“Sisemi kwamba wachezaji walioitwa sio wazuri la hasha! Ila kiuwezo katika mabeki wa pembeni walioitwa hakuna aliyenizidi,” alisema Kimenya.

Beki huyo alisema imefika hatua wachezaji wa timu ya Taifa wapatikane kutokana na uwezo wao na sio kukariri majina yale yale kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

“Timu ya Taifa ni ya wote na haipaswi hata wachezaji kujimilikisha jezi, mwenye kiwango kizuri kwa wakati fulani ndiye anapaswa kupewa nafasi na sio kukariri,” alisema Kimenya.

Kimenya ambaye alichaguliwa katika kikosi bora cha ligi msimu wa 2016/17 alisema ameshindwa kujiunga na timu za Simba na Singida United kwasababu hawajakubaliana kimaslahi.

“Simba walinifuata mara kadhaa lakini tulishindwa kufika muafaka kwenye maslahi Singida United pia hivyo hivyo kwahiyo nitaendelea kubaki Prisons, timu itakayonihitaji na kuniondoa kwenye ajira yangu iwe tayari kunilipa si chini ya Sh 50 milioni,”.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *