Kitaifa

Kinda Friends Awashangaza Simba Kurasini

on

Akram Msangi,Dar
MSHAMBULIAJI kinda Cliff Anthony amefunga mabao mawili ya ‘kideo’ wakati Friends Rangers ikiivimbia timu ya Simba kwa kuilazimisha sare ya mabao matatu katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

Cliff alifunga bao la kwanza kwa shuti kali nje ya 18 huku lile la pili akifunga kwa staili ya ‘tik tak’ kama alivyofanya mshambuliaji wa Juventus Mario Mandzukic jana kwenye mchezo wa fainali wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid. Bao jingine la Friends lilifungwa na Omari Wayne.

Simba ambayo inajiwinda na michuano mipya ya SportPesa Super Cup ilitumia wachezaji wengi wapya ambao wanatarajia kuwasajili na wengine wakiwa tayari wamesajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi mwezi Agosti.

Cliff Anthony (kushoto) akiwa na kikosi cha KMC walipopambana na Simba mwaka jana wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi. Cliff amekuwa akiisumbua ngome ya Simba kila anapokutananayo.

Katika mchezo huo uliokuwa mzuri kwa timu zote kushambuliana kwa zamu Simba ilipata mabao yake kupitia kwa Jamal Mnyate na Moses Kitandu aliyefunga mawili.

Wachezaji wapya waliochezea Simba kwenye mchezo huo na timu zao walizotoka kwenye mabano huo ni pamoja na Ahmad Msumi (Ndanda FC), Rashidi Mkoko (Mwadui FC), Yusuph Mlipili (Toto African) na Jamal Mwambeleko (Mbao FC).

Nyota watano wa Simba Mohammed Hussein, Ibrahim Ajib, Said Ndemla, Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin wapo nchini Misri katika kambi ya timu ya Taifa huku nahodha Jonas Mkude akibaki baada ya kupata ajali ya gari mwezi uliopita.

Simba itaanza kutupa karata yake siku ya Jumanne Juni 6 kwenye michuano ya SportPesa dhidi ya Nakuru All Stars.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *