Kimataifa

Kipa Genk Ashindwa Kuinusuru Australia

on

MOSCOW, Urusi
MLINDA mlango Mathew Ryan aliyekuwa akichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji kwa mkopo akitokea Valencia ameshindwa kulinusuru taifa lake la Australia na kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Ujerumani katika michuano ya kombe la mabara inayoendelea nchini Urusi.

Licha ya kuruhusu mabao hayo lakini Ryan aliweza kuhimili mikikimikiki ya washambuliaji wa Ujerumani waliokuwa wakiongozwa na nahodha Julian Draxler.

Mchezo huo ulikuwa ni pili wa kundi B baada ya jana Chile kuifunga Cameroon mabao 2-0 na kukaa kileleni mwa kundi hilo ikiwa na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa licha ya ushindi huo wa Ujerumani.

Ryan tayari amejiunga na timu ya Brighton & Hove Albion itakayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza msimu ujao baada ya kupanda daraja kutoka Championship.

Mabao ya Ujerumani katika mchezo huo yalifungwa na Lars Stindl, Draxler na Leon Goretza huku yale ya Australia yakifungwa na Tom Rogic na Tom Juric.

Ujerumani ilicheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza lakini Australia walicharuka baada ya kurudi mapumziko na kuliweka shakani lango la mabingwa hao wa dunia waliobebwa na umahiri wa mabeki wake.

Michuano hiyo itapumzika kwa siku ya kesho kabla ya kurejea keshokutwa kwa mechi za kundi A.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *