The sports Hub

Kiraka Simba atoa darasa la ubingwa

0 11

BEKI kiraka wa Wekundu wa Msimbazi Simba, Erasto Nyoni amedai kwamba ili kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara ‘TPL’ anatakiwa kujituma zaidi na kufuata maelekezo ya kocha ipasavyo ili kuepeuka kupoteza pointi katika mechi zilizosalia.

Alisema wanatakiwa kuzidisha ushirikiano na kupambana kwa nguvu zote katika michezo yote kutokana na ushindani uliyopo kwasasa kwa timu zinazotaka kutwaa ubingwa na nyingine zinazopambana kukwepa kutoshuka daraja.

“Muhimu ni kuzidi kushirikiana na kuongeza juhudi ili tuweze kupata pointi nyingine katika michezo inayokuja mbele yetu. Sisi ni mabingwa watetezi na tunahitaji tena kuchukua ubingwa wa msimu huu,’’ alisema.

Simba inayoshika nafasi ya tatu katika

msimamo wa ligi ikiwa na pointi 57, kesho saa 8 mchana itakuwa ikimenyana na wenyeji Coastal Union katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.