The sports Hub

Kitambi Aichambua Simba Nje, Ndani

0 758

KOCHA wa zamani wa Ndanda FC na Azam FC, Mtanzania, Denis Kitambi amewapa somo wachezaji wa Simba ili wafanikiwe kumyoosha Mwarabu Jumanne kwenye mchezo wa marudiano hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa.

Kitambi ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa kocha msaidizi wa Simba, amesema wachezaji wa Simba wanashindwa kupata matokeo kutokana na uzembe wawapo uwanjani kwani wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.

“Safu ya ushambuliaji inatakiwa iwe makini kumalizia mipira eneo la hatari, pia wachezaji wote kiujumla waache tabia ya kukaba kwa macho inaigharimu timu, ni wakati wao kupeperusha bendera ya Taifa,” amesema Kitambi.

Hata hivyo, Simba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza walipokuwa ugenini nchini Misri huku safu yao ya ulinzi ikionesha udhaifu baada ya kuruhusu mabao 10 katika mechi mbili.

 

Get real time updates directly on you device, subscribe now.