The sports Hub

Kiungo Yanga akunwa na uwezo wa Fei Toto

0 35

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Deo Lucas amemwangalia kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kisha akatamka dogo huyo anatakiwa kupambana ili aende kucheza soka la kulipwa Ulaya.

Lucas alisema anavutiwa na aina ya uchezaji  wa Fei na ni wakati wake wa kuhakikisha anapambana na kwenda kucheza soka la kulipwa na sio kubaki hapa Bongo kwani kiwango chake ni kikubwa hivyo kama akiendelea kukilinda basi muda si mrefu atapata timu ya kukipiga Ulaya kwani pia umri wake bado mdogo.

“Yanga wamepata bonge la kiungo ni mchezaji ambaye kwangu ni bora sana msimu huu japo haujaisha ila unaona tu mafanikio yake kwanza ameitwa timu ya taifa kwa kipindi kifupi hata umri wake bado mdogo hivyo hapo unaona mwanga mzuri kwake,”alisema Lucas.

Mchezaji huyo aliongeza kwa kusema Yanga ina viungo mafundi wengi

akiwepo Thaban Kamusoko, Said Makapu, Deus Kaseke, Pius Buswita, Raphael Daud lakini Fei amepata namba ya kudumu hivyo kikubwa kwake ni kuhakikisha anajituma ndani ya timu ili kumfanya aendelee kuwa katika ubora wake kitu ambacho kitamsaidia kuonekana na timu mbalimbali hapa duniani.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.