Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Kocha Kakamega Asema Simba ni Kubwa Sana Kwao

0 4,664

KOCHA mkuu wa Kakamega Home Boys ya Kenya, Paul Nkata amesema timu yake ni ndogo sana kwa Simba na kwamba wamekuja katika mashindano hayo kama washiriki na si washindani.

Akizungumza na wanahabari leo kwenye Hoteli ya Ole~Ken jijini Nakuru Nkata alisema timu yao no ndogo sana ukilinganisha na wapinzani wao Simba wanaotarajia kukutana nao katika mchezo wa nusu fainali kesho kwenye uwanja wa Afraha.

Related Posts
1 of 32

“Bado sijabadili kauli, sisi ni wadogo kwa Simba na tunalifahamu hilo. Simba ni mabingwa kule Tanzania wakati sisi tuko kwenye nafasi mbaya kabisa kwenye ligi yetu,” alisema.

Kakamega waliitoa Yanga kwa kuifunga mabao 3-1 kwenye mchezo wa robo fainali.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...