Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

KOCHA MASOUD: Nimeletwa Msimbazi na Mungu

Asema watu wa Simba ni watu wa mpira

0 1,326

BAADA ya leo timu ya Simba kuzidi kuwafurahisha mashabiki wake  kwa kuwachapa Singida United bao 1-0 hapo jana, kocha msaidizi Masoud Djuma ameelezea furaha yake na jinsi anavyojivunia kufanya kazi kwenye viunga vya Msimbazi huku akisema ujio wake ni mapenzi ya Mungu.

Masoud ambaye ni kipenzi cha mashabiki na wachezaji wa Wekundu hao amesema anajivunia kuwepo hapo kwasababu ilikua ni ndoto zake za siku nyingi ambapo amefunguka kitu kikubwa kinachompa furaha katika maisha yake ndani ya Simba ni jinsi wadau wa mabingwa hao wapya walivyo watu wa mpira wakiufatilia na kuupenda kwa dhati mchezo huo.

Related Posts
1 of 948

“Kwanza namshukuru Mungu mimi kuwepo hapa, naweza kusema mungu aliziona ndoto zangu za siku nyingi za kufanya kazi hapa na akaamua kuzitimiza, najivunia kufanya kazi na watu wa Simba kiujumla, wananifurahisha sana wanavyoupenda na kuufatilia mchezo wa soka.

Pia kocha huyo alifunguka jinsi anavyonufaika kufanya kazi na kocha mkuu Pierre Lechantre akisema ‘madini’ aliyonayo mfaransa huyo si ya mchezo.

“Lakini nafurahia sana kufanya kazi na makocha wenye ujuzi mkubwa zaidi yangu kama kocha mkuu Lechantre, najifunza vitu vingi na napata uzoefu kila siku,” alisema Masoud.

Masoud aliziteka nyoyo za mashabiki wa Msimbazi baada ya kuja na mfumo wake wa 3-5-2 ambao ulikifanya kikosi hicho kicheze soka la kasi huku wakifanikiwa kupata mabao mengi katika mechi zao. Hata hivyo kocha Lechantre alipokuja aliendelea na mfumo huo.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...