The sports Hub

KOCHA SIMBA: Baada Ya Al Ahly, Yanga Inafuata

0 39

KOCHA mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems ya ameweka wazi kuwa akili yake ipo kwenye mambo mawili tu kwa sasa ambayo ndiyo anayapa kipaumbele zaidi kwenye timu yake.

Aussems amesema kuwa licha ya kukabiliwa na mchezo mgumu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly lakini anachotakiwa ni kuhakikisha anachukua ubingwa wa msimu huu.

“Tuna mechi ngumu Jumanne ijayo lakini bado haiwezi kuwa kigezo cha kutufanya tuache kuangalia ligi ya kuu kwa sababu tunataka kutetea ubingwa wetu bila ya kuangalia nani yupo juu” alisema Aussems.

Mbali ya Simba kushiriki Ligi Mabingwa Afrika inakabiliwa na mechi saba za viporo katika Ligi Kuu Bara huku Yanga ikiongoza ligi kwa pointi 55, wakifuatiwa na Azam yenye pointi 48, huku Simba ikiwa na pointi 36.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.