The sports Hub

Kocha wa Samatta Apigwa Chini Misri

0 156

KLABU ya Al Ahly ya nchini Misri imemfukuza kazi kocha mkuu wa kikosi hicho Patrice Carteron baada ya muendelezo mbaya wa matokeo ya kikosi hicho.

Carteron ambaye aliwahi kuwafundisha Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wakiwa TP Mazembe ya DR Congo, amefukuzwa baada ya kikosi hicho kuboronga kwenye mashindano ya Arabs Club Championship na kupokea kipigo kwenye fainali ya Klabu Bingwa barani Afrika toka kwa Esperance ya Tunisia.

Carteron akitoa maelekezo kwa Samatta katika moja ya mechi alizoiongoza TP Mazembe

Akifundisha Mazembe kuanzia 2013-2016, kocha huyo alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika mara moja na Super Cup mara mbili lakini ameshindwa kutisha kwa waarabu hao ambao wameamua kumtimua akiwa hajatimiza hata mwaka tangu aanze kukifundisha kikosi hicho.

Carteron ameiongoza Al Ahly kwenye michezo 21 huku akishinda 12, sare tano na kupoteza michezo mitatu ukiwemo mchezo wa fainali.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.