The sports Hub

Kumbe ‘Kiburi’ cha Pluijm Mapinduzi Kinaanzia Hapa…

0 52

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Hans Pluijm amesema siri kubwa ya mafanikio ambayo timu yake inaendelea kupata katika michuano ya Kombe la Mapinduzi ni kuwajengea wachezaji wake hali ya kujiamini wanapokuwa uwanjani.

Pluijm ambaye alijiunga na Azam akitokea Singida United, alisema kuwa mchezaji mwenye kujiamini huwa na mbinu za ziada za kuwakabili wapinzani hata kama uwezo wake ni mdogo.

Hans Pluijm akimuongoza straika wake Obrey Chirwa kunyoosha misuli katika mazoezi ya leo kwenye uwanja wa Aaman.

Mkufunzi huyo wa soka aliendelea kusema, anafahamu changamoto zilizoko ndani ya uwanja hivyo katika kuhakikisha kikosi chake kinakuwa imara na kukabiliana na ushindani huo, anatumia muda mwingi kuwaandaa wachezaji wake kisaikolojia ili wajiamini zaidi.

“Tumeingia hatua ya nusu fainali ya Mapinduzi, hilo ni jambo zuri la kujivunia kuanzia benchi la ufundi, wachezaji hadi mashabiki. Kila mechi ni muhimu, kila mechi kwetu ni kubwa hivyo nimewaandaa vijana wangu kimwili na kiakili kuhakikisha tunapambana ili kushinda taji hili,” alisema Pluijm.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.