Kitaifa

Kwa maandalizi haya waleteni tu hao Amavubi

on

KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga ameridhishwa na maandalizi ya mchezo wa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi ya ndani (CHAN) dhidi ya Rwanda ‘Amavubi’ itakayofanyika leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Mayanga amewaambia Waandishi wa Habari kuwa amepata muda wa kutosha kuandaa vijana wake ambapo kama wataamka salama ana uhakika wa kufanya vizuri katika mchezo huo.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya Mtibwa Sugar amesema pia kutakuwa na mabadiliko kidogo katika kikosi kitachoshuka dimbani kesho kutokana na wachezaji wengine kuwa majeruhi na wale wasiokubalika kwa mujibu wa kanuni.

Kikosi cha Rwanda kinachotarajiwa kupambana na Stars leo

“Kiufundi kikosi kiko tayari kwa mchezo wa kesho (leo), tulipata siku za kutosha za maandalizi na kama tukiamka salama nina imani kubwa ya kuibuka na ushindi.

“Kutakuwa na mabadiliko kidogo ya wachezaji katika kikosi kilichoshiriki michuano ya COSAFA, nchini Afrika Kusini kutokana na kuwa majeruhi kama Mbaraka Yusuph wakati Thomas Ulimwengu na Elius Maguri hawatakuwepo sababu wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi,” alisema Mayanga.

Stars ipo jijini Mwanza katika Hoteli ya Isamilo tangu Jumatatu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ambapo wamefika mapema ili kuzoea mazingira ya uwanja CCM Kirumba utakaotumika leo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *