The sports Hub

Kwa Takwimu Hizi Guardiola Alistahili Zaidi ya Alichokipata

0 554

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola ametangazwa Kocha Bora wa Februari baada ya kuiongoza timu hiyo kuibuka na ushindi katika mechi zote nne walizocheza ndani ya mwezi huo.

Katika mwezi huo ambao Guardiola ametwaa tuzo yake ya sita ya kocha bora wa mwezi tangu ahamie Uingereza, City wamefanikiwa kufunga magoli 12 huku wao wakiruhusu goli moja tu.

City waliianza Februari wakiwa pointi tano nyuma ya vinara wa Ligi Kuu Uingereza, Liverpool lakini baada ya kuwabamiza Arsenal mabao 3-1 na Chelsea 6-0 mambo yakaanza kubadilika.

Vijana hao wa Guardiola waliendeleza maajabu kwa kwenda kuibanjua Everton mabao 2-0 kisha kumalizana na West Ham United nyumbani kwa kuwapiga bao 1-0.

Mhispania huyo amewabwaga kwa mara ya pili mfululizo Unai Emery na Ole Gunnar Solskjaer.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.