Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Licha Ya Ushindi, Manula Autema Ubingwa Hadharani

0 69
Related Posts
1 of 948Bakari Kagoma, Dar
GOLIKIPA namba moja wa klabu ya Azam Aishi Manula ambaye leo alikuwa nyota wa mchezo ameitoa timu yake katika kinyang’anyiro cha ubingwa baada ya kuzidiwa idadi kubwa ya pointi na vinara Simba.


Azam imefikisha pointi 34 kufuatia ushindi wa leo wa bao 1-0 dhidi ya Simba ambapo wamezidiwa alama 11 na Wekundu hao kitu kinachomtia shaka mlinda mlango huyo kwa timu yake kuwepo miongoni mwa wanaopigania ubingwa msimu huu.


Manula alisema itakuwa ngumu kwa Azam kuchukua ubingwa kwakuwa mzunguko wa kwanza wa ligi haukuwa mzuri kwao huku tofauti ya pointi baina yao na vinara Simba na ugumu wa ligi ulivyo kwa sasa ukiwaweka mbali na taji hilo.


“Japokuwa mpira una matokeo matatu lakini ndoto ya ubingwa kwa msimu huu inakuwa ngumu sana japokuwa tutaendelea kupambana hadi dakika ya mwisho,” alisema Manula.


Manula ambaye yupo kwenye kiwango bora kwa sasa alikuwa kikwazo kwa Simba kupata bao baada ya kuchomoa michomo mingi kutoka kwa washambuliaji wa Wekundu hao katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.


Manula amejihakikishia namba kwenye kikosi kwanza licha  ya timu hiyo kubadili  makocha mara kwa mara huku Mwadini Ally akikubali kukaa benchi ambapo katika msimu huu mlinda mlango huyo amedaka zaidi ya asilimia 98 ya mechi za Azam.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...