Kitaifa

Liuzio ataja kilichomzuia kwenda Sauzi

on

STRAIKA wa zamani wa ZESCO United ya Zambia aliyekuwa anakipiga kwa mkopo katika klabu ya Simba ameeleza sababu zilizomfanya asijiunge na kikosi hicho katika kambi ya nchini Afrika Kusini.

Simba waliondoka usiku wa kuamkia juzi na wanatarajiwa kukaa nchini humo kwa siku 14 kabla hawajarejea nchini kwa ajili ya tamasha la ‘Simba Day’ Agosti 8.

Akizungumza na BOIPLUS, Liuzio alisema mkataba wake wa mkopo ulishamalizika sambamba na ule wa ZESCO hivyo isingekuwa vema kuondoka wakati wapo kwenye mazungumzo na viongozi.

Wachezaji wa Simba wakiwa kambini Afrika Kusini

“Bado tupo kwenye mazungumzo na viongozi wa Simba kwa ajili ya kuingia mkataba mpya, yapo kwenye hatua za mwisho hivyo isingekuwa vizuri niondoke kabla ya kukamilisha jambo hili muhimu.

“Mungu akijali basi msimu ujao nitakuwa hapa Simba, litakuwa jambo zuri kwavile sasa nimezoeana na wenzangu utakuwa wakati wa kuisaidia timu kufanya vizuri,” alisema Liuzio ambaye hakuwa tayari kusema lini atasaini mkataba.

Hata hivyo chanzo chetu ndani ya klabu hiyo kimepasha kuwa muda wowote leo anaweza kusaini mkataba na kuondoka kwenda Sauzi kuungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *