Kitaifa

Liuzio atulizwa Simba, kutua Sauzi kesho

on

MSHAMBULIAJI Juma Liuzio amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu ya Simba msimu ujao.

Jana mtandao huu uliripoti kuwa straika huyo wa zamani wa Mtibwa ameshindwa kusafiri na timu kwenda kambini nchini Afrika Kusini kwavile alihitaji kumalizana na uongozi.

Simba imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wapya ikiwa ni sambamba na kuwabakiza wachezaji wao muhimu.

Juma Liuzio akiwa mazoezini Karume na kikosi cha Mtibwa Sugar

Liuzio ameonekana akifanya mazoezi na kikosi cha Mtibwa Sugar leo kwenye uwanja wa Karume ikiwa ni sehemu ya kujiweka ‘fit’.

Straika huyo ataondoka na ndege ya shirika la ndege la Rwanda usiku wa kuamkia kesho kupitia jijini Kigali kuelekea Sauzi ambako ataungana na wenzake walioweka kambi ya siku 14 kujiwinda na msimu mpya.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *