Kimataifa

Lukaku atupia tena United ikiiua City 2-0

on

CALIFORNIA, Marekani

MSHAMBULIAJI mpya wa Manchester United, Romelu Lukaku ameendelea kuwapa furaha mashabiki wa Mashetani hao baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika nchini Marekani.

Timu hizo zipo kwenye maandalizi ya msimu mpya wa ligi utakaoanza mwezi ujao ambapo miamba hiyo imeweka kambi nchini humo.

Lukaku alifunga bao hilo dakika ya 37 baada ya kumzidi ujanja mlinda mlango wa City, Ederson kufuatia mpira mrefu uliopigwa na kiungo Paul Pogba.

Dakika mbili baadae Marcus Rashford aliipatia United bao la pili baada ya kumalizia pasi ya Henrikh Mkhitaryan katikati ya walinzi wa City.

Hilo linakuwa bao la pili kwa Lukaku tangu ajiunge na United baada ya juzi kufunga moja katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi Salt Lake.

Lukaku amejiunga na United akitokea Everton kwa ada ya pauni 75 milioni mapema mwezi huu.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *