Kimataifa

Madrid yalambishwa tena mchanga Marekani

on

LOS ANGELES, Marekani
REAL Madrid imekubali kipigo cha pili ndani ya wiki moja kufuatia kuadhibiwa mabao 4-1 na Manchester City katika mchezo wa International Champions Cup nchini Marekani asubuhi ya leo.

Wikiendi iliyopita Real ilikubali kipigo kwa mikwaju ya penati 2-1 kutoka kwa Manchester United kufuatia sare ya bao moja hivyo kikosi cha kocha Zinedine Zidane kinamaliza michuano hiyo kwa kupepesuka.

City ilipata mabao yake kipindi cha pili kupitia kwa Nicholas Otamendi, Raheem Sterling, John Stones na Brahim Diaz huku bao la kufuatia machozi likifungwa na Oscar Rodriguez dakika ya 90.

Pamoja na kupata idadi hiyo kubwa ya mabao City pia walikuwa bora zaidi ambapo walilishambulia lango la mabingwa hao wa kihistoria wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya mara nyingi.

Katika michezo yote miwili Madrid walimkosa nyota wao Cristiano Ronaldo ambaye amepewa mapumziko maalum baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Mabara iliyofanyika nchini Urusi mwezi uliopita.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *