Kitaifa

Magufuli ‘Amlilia’ Ally Yanga, Kuzikwa Shinyanga Kesho

on

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa shabiki wa klabu ya Yanga Ally Mohammed ‘Ally Yanga’ kilichotokea mkoani Dodoma.

Ally alikutwa na mauti hayo jana katika eneo la Chipongolo wilaya ya Mpwapwa mkoani humo baada ya gari alilokuwa amepanda kupinduka na kusababisha kifo chake.

Ally Mohamed ‘Ally Yanga’ enzi za uhai wake

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu inasema Rais Magufuli anamkumbuka Ally katika ushiriki wake kwenye kampeni za Uchaguzi mkuu wa nchi mwaka 2015 baada ya kuzunguka nae katika maeneo mbalimbali kuhamasisha watu kukipigia kura chama chake.

Mbali na kuwa ni shabiki mkubwa na maarufu wa Yanga, Ally pia ni mwanachama safi wa chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye amekuwa akizunguka katika shughuli mbalimbali za kiserikali kama kukimbiza Mwenge na ziara za viongozi kitu kilichopelekea Rais kuguswa na msiba huo.

“Nimeguswa sana na kifo cha Ally Yanga, nilikuwa nae wakati wa kampeni za Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 alikuwa akihamasisha watu kukipigia kura chama changu. Pia amekuwa akiongoza mashabiki wenzake kuishabikia Yanga na timu ya taifa bila kuchoka. Kwa kweli alikuwa hodari sana katika ushabiki wake.”

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu, Ally atazikwa kesho huko Shinyanga.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *