Kitaifa

Mahakama yapiga chini kesi ya TPBO, PST, TPBL dhidi ya TPBC

on

MAHAKAMA kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi ya kampuni tatu zinazojihusisha na masuala ya ngumi kutokana na kutokidhi vigezo kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kampuni hizo ni Puglist Syndicate of Tanzania (PST), Tanzania Professional Boxing Organization (TPBO) na Tanzania Professional Boxing Limited (TPBL) ambazo zilifungua kesi kupinga kusajiliwa kwa kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBC) na kupewa majukumu ya kusimamia masuala yote ya ngumi za kulipwa nchini.

Kampuni hizo ziliungana kulitaka Baraza la michezo Tanzania (BMT) kutaja vigezo ilivyotumia kuipa usajili TPBC kusimamia ngumi za kulipwa kwakua hawana uwezo huo kisheria.

Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Temeke na katibu mkuu wa PST, Emmanuel Mrundwa lakini Mahakama hiyo ilishindwa kuisikiliza kutokana na kukosa nguvu kisheria.

Chaurembo Palasa (kushoto) akijadili jambo na Rais wa TPBO Yassin Abdallah ‘Ustadh’

Rais wa TPBC, Chaurembo Palasa amesema kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na Jaji Kihiyo imetupiliwa mbali kwani BMT ipo kwa mujibu wa sheria za nchi hivyo ilikuwa sahihi kuipa usajili wa TPBC kusimamia masuala yote ya ngumi za kulipwa.

“Kesi iliyofunguliwa kwa ajili ya kuhoji uwezo wa BMT kuipa usajili TPBC kusimamia ngumi za kulipwa nchini imetupiliwa mbali kutokana na kukosa vigezo kwa mujibu wa sheria,” alisema Palasa.

Kutokana na ombi lao kukosa vigezo vya kisheria Mahakama Kuu imeamua kuliondoa shauli hilo na kuwataka walalamikaji kulipa gharama za kesi hiyo ambazo hazijawekwa wazi kwakua zinaandaliwa na Mwanasheria mkuu wa Serikali.

Kutokana na kushindwa kwa kesi hiyo TPBC itabaki kuwa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania na sasa inapaswa kuendelea na mchakato wa kuwa na vyama vya Mikoa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *