Kitaifa

Majimaji yaanza usajili kwa kishindo, Tegete, Humud ndani

on

TIMU ya Majimaji jana Jumatatu iliwasainisha wachezaji 16 kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo msimu ujao huku nyota tisa wakiwa wapya wakiwemo Jerry Tegete (Mwadui), Abdulhalim Humud na Seleman Kassim Selembe (Stand United).

Nyota wengine wapya ni Danny Mrwanda, Jaffar Mohammed (Toto), Andrew Ntala (Prisons), Tumba Sued (Mbeya City), Sixnon Masekega, Mpoki Mwakinyukile na Saleh Malande (African Lyon). Wachezaji hao wamesaini mkataba wa mwaka mmoja kila mmoja.

Walioongezwa mikataba ni Peter Mapunda, Alex Kondo, Hashim Musa, Paul Maona, Yakob Kibiga, Kennedy Kipepe, Marcel Bonaventure.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu hiyo, Steven Ngonyani alisema kuwa wachezaji watatu Hassan Hamis, Idrisa Mohamed na Hashim Musa wapo katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kuwapa mikataba.

“Kuna wachezaji wengine tutawapandisha kutoka timu yetu ya vijana kwani tunahitaji kuwa na wachezaji 23 ambapo mazoezi rasmi yataanza Ijumaa wiki hii chini ya Kocha Msaidizi, Habibu Kondo,” alisema Ngonyani.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *