Kitaifa

Malinzi, Mwesigwa Wapata ‘Warithi’ TFF

on

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo na kumpitisha Wallace Karia (Makamu wa Rais) kuwa Kaimu Rais wa shirikisho hilo baada ya viongozi wakuu kushikiliwa na vyombo vya dola.

Kadhalika, Kamati hiyo ya imempitisha Mkurugenzi wa Ufundi wa Salum Madadi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF.

Wallace Karia

Viongozi hao watakaimu nafasi hizo tajwa hadi hapo mahakama itakapoamua kuhusu kesi zinazowakabili kwa sasa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Mwesigwa Celestine.

Kamati ya Utendaji ya TFF, imekutana kwa dharura kwa mujibu wa katiba ya shirikisho hilo Ibara ya 35 (1) inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6) na kufanya uamuzi huo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *