Kimataifa

Man City, Barca zatisha Marekani

on

MIAMI, Marekani
TIMU za Barcelona na Manchester City zimeshinda mechi zake za kirafiki za maandalizi ya msimu mpya wa ligi zinazoendelea nchini Marekani usiku wa kuamkia leo.

Barcelona imewafunga mahasimu wao wakubwa Real Madrid mabao 3-2 ikiwa ni El Classico ya kwanza kwa kocha Ernesto Valverdo wa Barca mtanange ambao huvuta hisia za mashabiki wengi duniani.

Gerrard Pique akishangilia bao la ushindi

Katika mchezo huo uliokuwa mkali kwa muda wote mabao ya Barcelona yalifungwa na Lionel Messi, Ivan Rakitic na Gerrard Pique wakati ya Real yakiwekwa kimiani na Mateo Kovacic na Marco Ansencio.

Valverde ameiongoza Barca kushinda mechi zote tatu za maandalizi ambapo aliifunga Juventus (2-0), Manchester United (1-0) na ushindi wa jana dhidi ya Real.

Mchezo mwingine uliopigwa kwenye mji wa Nashville, City ilitoa kipigo cha mabao 3-0 kwa Tottenham Hotspur katika mchezo wa kujipima nguvu ambapo vijana wa Pep Guardiola wameonyesha msimu huu wamejidhatiti kufanya vizuri.

 

Huu ni ushindi wa pili mkubwa mfululizo kwa City baada ya wiki iliyopita kuifunga Real Madrid mabao 4-1 na kuzitumia salamu timu zinazoshiriki ligi kuu nchini Uingereza.

Mabao ya City yalifungwa na John Stones (10), Raheem Sterling (72) na Brahim Diaz (90).

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *