Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Manara Ataja Sababu za Kuishangilia Singida United

0 5,434

MSEMAJI wa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Simba SC, Haji Manara  amesema alikuwa na furaha baada ya Singida United kuiondosha AFC Leopards kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup kwa mikwaju ya penati kwa sababu ameanza kuona dalili za kulipa kisasi.

Manara ambaye alikuwa uwanjani pamoja na baadhi ya wachezaji wa Simba wakishuhudia mpambano huo alisema anatamani kuona timu za Tanzania zikicheza fainali ya michuano hiyo kama ambavyo Wakenya walifanya mwaka jana nchini Tanzania.

Related Posts
1 of 32

“Kwanza kabisa ni utanzania, lazima niishangilie timu ya kwetu Tanzania lakini pia hawa jamaa walipokuja kwetu walicheza fainali wenyewe kwa wenyewe pale uwanja wa Taifa, sasa kama wao waliweza kwetu kwanini sisi tushindwe hapa kwao?, tunataka kucheza fainali na Singida hapa,” alisema Manara.

Msemaji huyo asiyeshindika kirahisi kwa maneno akiwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully na baadhi ya wachezaji walishuka chini kuwapongeza wachezaji na makocha wa Singida mara baada ya mchezo huo kumalizika ikiwa ni ishara ya kuwaunga mkono kwa kile walichokifanya.

Singida sasa watakutana na Gor Mahia katika mechi ya nusu fainali huku Simba wenye wakisubiri kupepetana na Kakamega Home Boys Alhamisi hii kwenye uwanja wa Afraha uliopo jijini Nakuru.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...