The sports Hub

Masharti Aliyotoa Zidane Kabla ya Kusaini Tena Madrid

0 551

KOCHA Zinedine Zidane ‘Zizou’ amerejea Real Madrid na ataanza majukumu ya kukinoa kikosi hicho leo, hiyo ikiwa ni baada ya Santiago Solari kutupiwa virago hapo jana.

Hata hivyo kurejea kwa mfaransa huyo kuliambatana na mambo kadhaa ya kusisimua ikiwemo suala la masharti aliyoyatoa kwa Rais wa klabu, Florentino Perez kabla ya kusaini mkataba huo utakaodumu hadi 2022.

Zidane ametaka mambo yafuatayo yafanyike ili kazi yake iwe yenye mafanikio kwa mara nyingine;

1) Ametaka kupewa mamlaka makubwa ya kuamua kila kitu katika kikosi.

2) Ameitaka Madrid kuuza wachezaji wote ambao yeye hawahitaji.

3) Kusitisha mpango wa kuwauza Marcelo na Isco kwani ni katika wachezaji anaowahitaji kikosini.

4) Hataki Neymar anunuliwe kikosini hapo.

5) James Rodriguez asirejeshwe tena kama ambavyo ilikuwa ikitajwa.

6) Zifanyike jitihada za dhati za kumnunua Kylian Mbapp√© 

Get real time updates directly on you device, subscribe now.