Kitaifa

Maslahi Kiduchu yamkimbiza Kaseke Yanga

on

Akram Msangi, Dar
KIUNGO Deus Kaseke ametaja sababu za kutimka Yanga na kujiunga Singida United kuwa ni maslahi kwakua mabingwa hao wameshindwa kumpa alichokuwa akihitaji huku akitanabaisha kuwa mpira ndiyo kazi inayoendesha maisha yake.

Kaseke ambaye mkataba na mabingwa hao umemalizika amekuwa kwenye mazungumzo yakuongeza kandarasi mpya kwa wiki kadhaa lakini katika upande wa maslahi walishindwana kabla ya kuamua kutimkia Singida United.

Mchezaji huyo wazamani wa Mbeya City amesaini mkataba wa miaka miwili jana na timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu ambayo imejipanga kufanya vizuri kutokana na usajili unaoendelea kufanya.

Kaseke ameiambia BOIPLUS kuwa hakuwa na chaguo zaidi ya kusaini Singida kutokana na dau alilotengewa akilinganisha na kiasi ambacho angekipata kama angeendelea kubaki Yanga.

“Mpira ni kazi, kilichonisukuma kujiunga na Singida ni maslahi Yanga wameshindwa kunipa nilichokuwa nahitaji hilo tu. Ila nawapenda mashabiki wa Yanga kwa ushirikiano walionipa ila watambue mpira ni kazi kama zilivyo kazi nyingine,” alisema Kaseke.

Kaseke anakuwa mchezaji wa pili kutoka Yanga kujiunga na Singida ndani ya wiki moja baada ya mlinda mlango Ally Mustaph ‘Barthez’ kufanya hivyo mwanzoni mwa wiki.

Singida ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa yakufanya vizuri katika ligi msimu ujao kutokana na usajili uliofanya mpaka sasa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *