Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

MASOUD DJUMA: Nimeongeza Kitu Kimoja tu Simba

0 3,231

KOCHA msaidizi wa klabu ya Simba, Masoud Djuma amesema alifanya jambo moja tu kwenye kikosi hicho kuelekea mchezo wa nusu fainali walioshinda kwa penati 5-4 dhidi ya Kakamega Homeboys hiyo ikiwa ni baada ya kocha mkuu Pierre Lechantre kuwekwa pembeni na uongozi.

Masoud ameiongoza timu hiyo kutinga fainali ya michuano ya Sportpesa Super Cup wakati Lechantre akiwa jukwaani huku taarifa zikidai mfaransa huyo hana chake tena kwa wekundu hao.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya mchezo huo, Masoud alisema alichofanya yeye ni kuwajenga kisaikolojia ili wajiamini zaidi jambo ambalo alisema hawakuwanalo kwenye mechi ya robo fainali.

Related Posts
1 of 32

“Nimefanya kitu kimoja tu, kuwajengea kujiamini, walicheza mchezo wa kwanza wakionekana hawana morali kama vile walitaka watolewe tu, kwahiyo nikazungumza nao na umeona walivyocheza leo,” alisema.

Akizungumzia suala la kuchukua kiti cha Lechantre raia huyo wa Burundi alisema hilo ni suala la uongozi halimhusu yeye na kwamba walichofanya leo ni kuhakikisha hawapotezi mchezo kwa heshima ya mfaransa huyo.

“Hayo waulize viongozi mimi sihusiki nayo, nipo hapa kama kocha msaidizi na leo tulicheza kwa bidi kwa heshima ya kocha wetu ambaye alikuwa jukwaani ndio sababu baada ya mechi tulienda kumshukuru.”

Simba sasa itapambana na mshindi kati ya Gor Mahia na Singida wanaopambana muda huu kwenye uwanja wa Afraha.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...