The sports Hub

Matola aipa neno Simba

0 8

Wakati Simba ikiikabili TP Mazembe kwenye mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kocha wa Lipuli ya Iringa, Selemani Matola amesema jambo la kwanza wachezaji wanatakiwa kujitambua na kujua thamani yao ili kuibeba Simba katika mchezo huo.

Nahodha huyo wa zamani wa klabu hiyo amesema Simba inacheza vizuri lakini wapo taratibu na wanapiga pasi nyingi za taratibu hilo ni tatizo ambalo kocha anatakiwa kuliangalia kwa jicho la tatu na kulifanyia kazi, vinginevyo hali inaweza kuwa mbaya huko DR Congo.

 “Pia tatizo lingine la Simba liko katika safu ya ulinzi wanatakiwa kubadilika, timu inaposhambuliwa inatoa nafasi kwa wapinzani kufika golini mara kwa mara,”alisema Matola.

Licha ya kutoka sare katika mchezo wa

awali, Matola amesema TP Mazembe ni timu bora Afrika lakini Simba ina nafasi ya kufanya vyema endapo itatumia mbinu ya kushambulia, kukaba kwa pamoja na kutoiruhusu Mazembe kumiliki mpira.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.