Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Maumivu ya Goti Yamweka nje Manula

0 732

KIPA namba moja wa Simba, Aishi Manula ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake asubuhi ya leo akiugulia maumivu ya goti baada ya kugongana na beki Paul Bukaba katika mchezo wa jana dhidi ya Kariobangi Sharks.

Manula alilazimika kutibiwa kwa dakika kadhaa uwanjani kabla hajaendelea na mchezo lakini akionekana kutokuwa sawa ambapo baada ya mchezo huo alikuwa akitemebea kwa kuchechemea.

Related Posts
1 of 32

Kinda Salim Ally ndiye kipa pekee aliyefanya mazoezi leo ingawa meneja wa Simba, Richard amesema daktari wa timu hiyo Yassin Gembe anapambana kuhakikisha kipa huyo anakuwepo uwanjani kwenye mchezo ujao wa nusu fainali hapo keshokutwa.

Kama Aishi Manula atashindwa kukaa langoni katika mchezo wa Alhamisi dhidi ya Kakamega Home Boys basi kinda huyu Salim Ally ndiye atakayebeba jahazi

Kwa upande wake Bukaba amefanya mazoezi vizuri ingawa alionekana akiwa amefungwa bandeji kwenye goti. Hata hivyo wawili hao walionekana jioni hii kwenye dimba la Afraha wakishuhudia pambano la AFC Leopards dhidi ya Singida United.

Simba itapambana na Kakamega Home Boys Juni 7 kwenye uwanja wa Afraha kuwania kucheza fainali ya michuano hiyo dhidi ya mshindi kati ya Singida na Gor Mahia ambapo bingwa atazawadiwa kikombe pamoja na kitita cha dola 30,000.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...