Kitaifa

Mayanga Awachinjia Baharini Nyota Wanne Simba

on

NYOTA wanne wa timu wa Simba wamepigwa panga kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kitakachoshiriki michuano iliyoandaliwa na Baraza la Michezo la nchi za Kusini mwa Afrika (COSAFA) itakayofanyika nchini Afrika Kusini baada ya kikosi hicho kufanyiwa marekebisho.

Nyota wa Simba ambao kocha wa timu hiyo Salum Mayanga amewaengua kwenye kikosi hicho kitachoingia kambini Jumapili Juni 18 kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ni Ibrahim Ajib, Jonas Mkude, Said Ndemla na Mohamed Hussein ambaye ni majeruhi.

Nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta nae hakujumuishwa kwenye kikosi hicho huku Elius Maguri na Stamili Mbonde wakiongezwa kwenye safu ya ushambuliaji.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 25 ambapo Stars ambayo ni timu mwalikwa imepangwa kundi A sambamba na timu za Mauritius, Malawi na Angola wakati kundi B kuna timu za Msumbiji, Shelisheli, Zimbabwe na Madagascar.

Kikosi kamili kilichotangazwa leo kinaundwa na makipa Aishi Manula (Azam FC), Benno Kakolanya (Yanga) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Walinzi ni Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Erasto Nyoni (Azam FC), Hassan Ramadhan ‘Kessy’ (Yanga) Amim Abdulkarim (Toto Africans), Salim Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons).

Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Salmin Hoza (Mbao FC),
Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya (Simba), Simon Msuva (Yanga), Raphael Daudi (Mbeya City).

Safu ya ushambuliaji itaongozwa na Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna- Sweden), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar) na Shabani Idd (Azam FC).

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *