Kitaifa

MAYANGA: Ubora wa Kambi Hii Utaimaliza Lesotho

on

ALEXANDRIA, Misri
KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Taifa ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga amefurahishwa na mazingira ya kambi waliyoweka katika mji wa Alexandria nchini Misri ambapo amekiri itakuwa na manufaa makubwa kuelekea mchezo wao ujao.

Stars imeweka kambi nchini humo kujiwinda na mchezo wa kufuzu michuano ya Afrika (AFCON) dhidi ya Lesotho mtanange utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Juni 10.

Mayanga alisema wachezaji wapo katika mazingira tulivu na programu zikiendelea kama zilivyopangwa huku afya za nyota hao zikiwa zimeimarika pasipo na shaka yoyote.

“Mazingira ya kambi ni mazuri na rafiki kwa wachezaji wetu na hali zao ni nzuri wanaendelea na program za mazoezi kama tulivyopanga,” alisema Mayanga.

Stars inatarajia kurejea nchini Juni 7 tayari kwa mechi hiyo siku tatu mbeleni ambapo kocha Mayanga alisema dhamira yake ni kushinda michezo yote ya nyumbani ili kujiweka kwenye mazingira ya kufuzu fainali hizo.

Stars ipo kundi L pamoja na timu za Uganda, Cape Verde na Lesotho. Mshindi wa kundi hilo atafuzu moja kwa moja katika michuano hiyo itakaofanyika nchini Cameroon mwaka 2019.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *