Kitaifa

Mbeya City wamalizana na kiungo wa Simba SportPesa

on

KLABU ya Mbeya City imeendelea kuimarisha kikosi chake baada ya kufanikiwa kupata saini ya kiungo Bakari Masoud kwa mkataba wa miaka miwili.

Bakari aliyewahi kuzitumikia timu za Coastal Union, Yanga na Fanja ya Oman amejiunga na City akiwa mchezaji huru kutokana na kutokuwa na timu katika kipindi hiki.

Kiungo huyo alioneka kwenye kikosi cha timu ya Simba kilichoshiriki michuano ya SportPesa iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwezi Juni mwaka huu.

Wagonga nyundo hao wa jiji la Mbeya waliachana na nahodha wao Kenny Ally aliyejiunga na Singida United hivyo kusajiliwa kwa Bakari huenda kukaimarisha tena safu ya kiungo ya timu hiyo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *