Kitaifa

Mbeya City Yachomoa ‘Kitasa’ Kagera Sugar

on

BEKI wa kati wa Kagera Sugar Erick Kyaruzi ‘Mopa’ ameachana na Wakata miwa hao na kujiunga na timu ya Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

Kyaruzi ambaye alijiunga na Kagera akitokea Toto African mwaka 2012 amekuwa na msimu mzuri kitu kilichowafanya City kugonga hodi kwa Wakata miwa na kuipata saini yake.

Beki huyo ameiambia BOIPLUS kuwa anaamini uwezo wake akiunganisha na wachezaji atakaokutana nao kutaifanya City kurejesha makali yaliyopotea kwa misimu miwili sasa.

Akizungumzia kuyumba kwa timu ya Mbeya City huku akitokea kwenye timu iliyomaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo Kyaruzi alisema katika mpira wa miguu kuna kipindi kinakuwa kigumu ila amejipanga kuhakikisha anaisadia kufanya vizuri msimu ujao.

“Nimejiunga na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu, naamini uwezo wangu nikishirikiana na wenzangu tunaweza kuisaidia timu kufanya vizuri msimu ujao,” alisema Kyaruzi.

City ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya 11 baada ya kujikusanyia pointi 33 ambapo ilikuwa miongoni mwa timu ambazo zilikuwa kwenye hati hati ya kushuka daraja hali iliyowafanya viongozi wa Wagonga nyundo hao wa Mbeya kutafuta wachezaji wazuri ili kukisuka upya kikosi chao.

Dirisha la usajili limefunguliwa Juni 15 ambapo timu zote zimekuwa zikifanya jitihada za kuimarisha vikosi vyao kwa ajili ya msimu mpya wa ligi mwezi Agosti.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *