The sports Hub

MENEJA YANGA: Tutabeba Makombe Mawili Msimu Huu

0 28

MENEJA wa timu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanachukua m akombe mawili mwaka huu, kuanzi kombe la ligi kuu hadi Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Cannavaro, alisema pamoja na kukabiliwa na ugumu wa kiuchumi, lakini haizuii kufanya vizuri katika mechi za ligi kuu bara na FA.

”Malengo yetu mwaka huu ni kupata ubingwa wa pande zote. Kama unavyoona kwa sasa hatuna muda wa kupoteza na hatupo tayari kufungwa na timu yoyote, ” alisema nahodha huyo wa zamani wa Yanga.

Alisema kutokana na ubora wa kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, kwa sasa wapo katika mkakati mzito wa kupata ushindi kila mchezo watakaocheza.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.