Kitaifa

MIGI: Ligi ya Kenya isikieni tu

on

KIUNGO wa zamani wa timu ya Azam FC anayechezea Gor Mahia Jean Babtiste Mugiraneza ‘Migi’ amesema kuwa ligi ya Kenya ni bora ukilinganisha na ya Tanzania.

Kiungo huyo ambaye alikuwepo kwenye kikosi cha Gor kilichopokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Everton jioni ya leo kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam amesema ligi ya Kenya ni bora kutokana na wachezaji wake kujitambua zaidi tofauti na Tanzania.

Migi raia wa Rwanda amesema amecheza ligi ya nyumbani kwao, Tanzania na sasa yupo Gor lakini amegundua ligi ya Kenya ni bora ukilinganisha na hizo kuanzia uongozi wa klabu, wachezaji na chama cha soka.

“Ni rahisi kumkuta mchezaji anajifua peke yake bila kumsubiri kocha au kipindi ligi inapomalizika, ndiyo maana wachezaji wanakuwa fiti muda mrefu na kuifanya ligi kuwa ngumu.

“Ukiangalia kikosi cha Gor kilichobeba ubingwa wa SportPesa wachezaji wengi walikuwa wanatumikia timu zao zaTaifa lakini waliokuwepo waliweza kufanya vizuri kwakua walikuwa fiti. Ukiangalia mchezo wa leo tumepoteza ila tulicheza vizuri,” alisema Migi.

Kiungo huyo amesema kupitia mchezo dhidi ya Everton wamejifunza mambo mengi kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo kama Wayne Rooney, Leighton Bainnes, Kelvin Mirallas na wengine ambao yatawajenga na kuwasaidia kufanya vizuri kwenye ligi ya Kenya.

“Ilikuwa ni jambo zuri kucheza na wachezaji wenye viwango bora duniani kama Rooney, tumejifunza mambo mengi ambayo tutayafanyia kazi tukifika nyumbani,” alisema Migi.

Katika mchezo huo mabao ya Everton yalifungwa na Rooney na Kierdin Dowell huku lile la Gor likifungwa na Tuyisenge Jacquer.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *