The sports Hub

Mkongomani Yanga azitaka pointi tatu za Mtibwa

0 7

KOCHA mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa ili kikosi chake kiweze kupata pointi tatu kesho mkoani Morogoro mbele ya Mtibwa Sugar ni lazima wachezaji wake wacheze kwa kiwango cha juu mchezo huo.

Mkongomani huyo ameleza kwamba hana cha kuhofia kwa sasa licha ya kuwakosa wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza kiungo Feisal Salum mwenye kadi tatu za njano na beki wa kati Kelvin Yondani mwenye kadi nyekundu.

. “Ili ushinde mechi unatakiwa kufunga mabao na hilo halijalishi unacheza na timu ya aina gani. Mtibwa ni timu imara inayoundwa na wachezaji vijana na wakongwe hivyo mchezo utakuwa ni mgumu lakini tucheze kwa kiwango cha juu zaidi ya tulivyofanya kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar,” alifafanua.

Yanga yenye pointi 74 itashuka uwanja wa

Jamhuri, Morogoro ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda mchezo wa kwanza uliochezwa Taifa kwa mabao 2-1.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.